Matthew 14:22-27

22 aMara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 23 bBaada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Isa alikuwa huko peke yake. 24Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.

25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,
Zamu ya nne ya usiku ni kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi.
Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji.
26 dWanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.

27 eLakini mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”

Copyright information for SwhKC